Bonyeza Hapa - Alhidaaya.com

Transkript

Bonyeza Hapa - Alhidaaya.com
VIPI UWEZE KUHIFADHI QUR-AAN?
Ummu Iyyaad:
1
www.alhidaaya.com
01- Yaliyomo
02- Utangulizi
03- Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan
04- Umri Bora Wa Kuhifadhi Qur-aan
05- Nasaha Za Kuhifadhi Qur-aan
06- Utaratibu Wa Kuhifadhia Qur-aan
07- Zingatia Aayah Zinazofanana
08- Kuithibitisha Qur-aan Baada Ya Kuihifadhi
09- Hitimisho:
2
www.alhidaaya.com
02-Utangulizi:
Qur-aan, maneno ya Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬, Aliyopelekewa Wahyi
Mtume (‫ )صلى ﷲ عليه وآله وسلم‬kupitia Jibriyl ‘alayhis-salaam,
akawasomea Maswahaba, nao wakawasomea waliofuatia,
ikaendelea kusomwa na kufundishwa hadi kutufikia sisi. Ni Hidaaya
kwetu, ni Nuru inanawirisha nyoyo zetu, ni kamba nene
inayounganisha Waislamu, ni miyzani ya uadilifu, ni poza ya moyo
ya kila aina ya maradhi; kufru, shirki, unafiki, uhasidi, uchoyo na
inatibu kila aina ya maasi na maovu. Imejaa hikma katika Aayah
zake, Shari’ah zake ambazo zinamfaa bin-Aadam wakati wowote,
zama zote, na popote alipo. Amri na makatazo Yake Allaah ( ‫سبحانه‬
‫ )وتعالى‬humo pamoja na kumtii Mtume (‫ )صلى ﷲ عليه وآله وسلم‬ni sababu
ya furaha na kufaulu kwa binaadamu katika dunia yake na Akhera
yake. Anasema Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬:
×πuΗ÷qu‘uρ “Y‰èδuρ Í‘ρ߉Á9$# ’Îû $yϑÏj9 Õ!$xÏ©uρ öΝà6În/§‘ ÏiΒ ×πsàÏãöθ¨Β Νä3ø?u!$y_ ô‰s% â¨$¨Ζ9$# $pκš‰r'¯≈tƒ 
〈 ∩∈∇∪ tβθãèyϑøgs† $£ϑÏiΒ ×ö&yz uθèδ (#θãmtøu‹ù=sù y7Ï9≡x‹Î7sù ϵÏFuΗ÷qtÎ/ρu «!$# È≅ôÒxÎ/ ö≅è% ∩∈∠∪ tÏΨÏΒ÷σßϑù=Ïj9
Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni Mawaidha (Qur-aan
inayoamrisha mema na kukataza maovu) kutoka kwa Mola wenu,
na Shifaa (poza) ya yale (maradhi) yote yaliyomo vifuani, na
Hidaayah na Rahmah kwa Waumini. Sema: (ee Muhammad ): “Kwa fadhila za Allaah na kwa Rahmah Yake (Qur-aan,
Uislamu, Iymaan), basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko
wanayoyakusanya (mali na starehe za dunia)1.
Lakini manufaa na fadhila hizo haziwezi kumfikia mtu isipokuwa kwa
atakayeisoma Qur-aan kwa njia itakayomridhisha Allaah ( ‫سبحانه‬
‫)وتعالى‬, Naye Anasema:
1
Yuwnus (10: 57-58)
3
www.alhidaaya.com
〈 3 ϵÎ/ tβθãΖÏΒ÷σムy7Íׯ≈s9'ρé& ÿϵÏ?uρŸξÏ? ¨,ym …çµtΡθè=÷Gtƒ |=≈tGÅ3ø9$# ãΝßγ≈oΨ÷-s?#u tÏ%©!$# 
Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ya kukisoma kwake
(ipasavyo); hao ndio wanaokiamini2
Kitabu hiki In Shaa Allaah, kitaweza kumsaidia anayetaka kuhifadhi
Qur-aan pindi mtu akiweka azimio la nguvu na kuanza kwanza
Niyya safi moyoni, kuomba du’aa, kufanya juhudi kubwa,
kuendelea nayo hifdhi yake bila ya kukata tamaa na kuithibitisha
baada ya kuihifadhi. Hapo ndipo itakapomthibitikia kauli ya Allaah
( ) iliyokariri mara nne katika Suwratul-Qamar:
〈 ∩⊇∠∪ 9Ï.£‰•Β ÏΒ ö≅yγsù Ìø.Ïe%#Ï9 tβ#uöà)ø9$# $tΡ÷œ£o„ ô‰s)s9uρ 
(Na kwa yakini Tumeifanya Qur-aan sahali kuikumbuka [kuisoma,
kuihifadhi na kuifahamu], basi je, yuko yeyote anayekumbuka [na
kuwaidhika?))]3
Namuomba Allaah ( ) Ajaalie kazi hii iwe kwa ajili ya kupata
Radhi Zake Pekee na Ajaalie iwe yenye manufaa kwa ndugu zetu
wa Kiislamu na namuomba Atughufurie na Atusamehe kwa makosa
yoyote yatakayokuwemo.
Wa-Swalla-Allaahu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Swahbihi
wa sallam.
Ummu Iyyaad–Talha Muhammad Al-Haamid Abu Bakr bin Saalim
20 Rabiy’ul Awwal 1434– 2 Februari 2003
2
3
Al-Baqarah (2: 121)
Al-Qamar: (54: 17, 22, 32, 40)
4
www.alhidaaya.com
03- Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan
Allaah Amewafanyia wema mkubwa na ihsaan Waumini kwa
kuwaletea Maneno Yake Mwenyewe kwa namna ya kuweza
kusomeka na kusikilizika Aayah Zake, na kufikia kumpelekea
msomaji au msikilizaji kuhisi kuwa anasemeshwa na Muumba wake
na kumsikiliza. Hili ndilo linaloipa na kuitunuku Qur-aan nafasi
isiyokadirika kwa Muumini kwani wote wanaamini kuwa Qur-aan ni
Maneno ya Allaah yaliyoteremshwa kwa Mtume ( )
kupitia kwa Jibril ( !" ) na kusomwa kwake ni ‘ibaadah.
Moja kati ya amri tatu alizoamrishwa Mtume ( ) na
Allaah kama inavyobainisha Qur-aan katika Aayah ya SuwratunNaml ni kuisoma Qur-aan. Anasema Allaah (#$ %#&):
y Ρ¯ )Î
zΒÏ β
t θ.ä &r β
÷ &r N
ß ö ΒÏ &é ρu ( & 
ó «
x ≅
‘ 2
à
…&ã !s ρu $γ
y Βt § m
y “%
Ï !© #$ οÍ $
t #ù 7t 9ø #$ νÍ ‹
É ≈δ
y U
& ‘u ‰
y 6ç ã
ô &r β
÷ &r N
ß ö ΒÏ &é $! ϑ
(β
t #u ö )
à 9ø #$ #( θu =è ?ø &r β
÷ &r ρu ∩⊇∪ 
t ϑ
Ï =Î ¡
ó ϑ
ß 9ø #$
(([Sema ee Muhammad ] “Hakika nimeamrishwa
nimwabudu Mola wa huu mji [Makkah] Ambaye Ameufanya
mtakatifu [kwa Amri Yake]. Naye ni Vyake Pekee kila kitu. Na
nimeamrishwa kwamba niwe
miongoni
mwa Waislamu”
[wanaojisalimisha]. Na kwamba nisome Qur-aan”))4
Akaamrishwa tena kwamba:
( οn θ4 =n Á
¢ 9#$ Ο
É %Ï &r ρu =
É ≈Gt 3
Å 9ø #$ ∅
š
ΒÏ 7
y ‹ø 9s )Î 
z r
Ç ρ&é $! Βt ≅
ã ?ø #$
((Soma [ee Muhammad ] uliyofunuliwa Wahyi kwako
katika Kitabu [Qur-aan] na simamisha Swalaah))5
Japokuwa Qur-aan iliteremshwa kwake ( ), bila shaka
Waumini wanaingia katika hilo.
4An-Naml:
(27: 91-92)
(29: 45)
5Al-‘Ankabuut
5
www.alhidaaya.com
Katika majukumu mengine aliyopewa Mtume ( ) kwa
Waumini yenye kufungamana na Qur-aan baada ya kutakiwa
kuisoma yeye mwenyewe ( ), ni kuwasomea na
kuwafunza kuweza kuisoma Qur-aan kama alivyosomewa. Allaah
(#$ %#&) Ametaja hilo katika Aayah tatu zilizofanana takriban kwa
ukaribu sana, na ya nne ni du’aa ambayo baba wa Mitume Nabii
Ibraahiym ( !" ) alikuwa akiiomba na Allaah ( ) kwa
Rahmah na Fadhila Zake Akaitakabali na matokeo yake ni kuletwa
kwetu Mtume Muhammad ( ): Anasema Allaah ( %#&
#$):
y7¨ΡÎ) 4 öΝÍκ@Ïj.t“ãƒuρ sπyϑõ3Ïtø:$#uρ |=≈tGÅ3ø9$# ÞΟßγßϑÏk=yèãƒuρ y7ÏG≈tƒ#u öΝÍκö@n=tæ (#θè=÷Gtƒ öΝåκ÷]ÏiΒ Zωθß™u‘ öΝÎγ‹Ïù ô]yèö/$#uρ $uΖ−/‘u
∩⊇⊄∪ ÞΟŠÅ3ysø9$# Ⓝ͕yèø9$# |MΡr&
((Mola wetu, Peleka kwao Mtume miongoni mwao ataewasomea
Aayah Zako na ataewafunza Kitabu na Hikmah na
atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Al-’Aziyzul-Hakiym [Mwenye
Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima - Mwenye Hikma wa yote
daima])).” 6
|=≈tGÅ3ø9$# ãΝà6ßϑÏk=yèãƒuρ öΝà6ŠÏj.t“ãƒuρ $oΨÏG≈tƒ#u öΝä3ø‹n=tæ (#θè=÷Gtƒ öΝà6ΖÏiΒ Zωθß™u‘ öΝà6‹Ïù $uΖù=y™ö‘r& !$yϑx.
∩⊇∈⊇∪ tβθßϑn=÷ès? (#θçΡθä3s? öΝs9 $¨Β Νä3ßϑÏk=yèãƒuρ sπyϑò6Ïtø:$#uρ
((Kama Tulivyomtuma kwenu Mtume anayetokana na nyinyi,
anawasomea Aayah Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni
Kitabu na Hikmah, na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa
mkiyajua))7
6Al-Baqarah:
7
(2: 129)
Al-Baqarah (2: 151)
6
www.alhidaaya.com
öΝÍκ@Åe2t“ãƒuρ ϵÏG≈tƒ#u öΝÍκö@n=tæ (#θè=÷Gtƒ ôΜÎγÅ¡àΡr& ôÏiΒ Zωθß™u‘ öΝÍκ@Ïù y]yèt/ øŒÎ) tÏΖÏΒ÷σßϑø9$# ’n?tã ª!$# £tΒ ô‰s)s9
∩⊇∉⊆∪ AÎ7•Β 9≅≈n=|Ê ’Å∀s9 ã≅ö6s% ÏΒ (#θçΡ%x. βÎ)uρ sπyϑò6Ïtø:$#uρ |=≈tGÅ3ø9$# ãΝßγßϑÏk=yèãƒuρ
((Kwa yakini Allaah Amewafadhilisha Waumini pale Alipomtuma
miongoni mwao Mtume kutokana na nafsi zao; anawasomea
Aayah Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah;
japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana))8
sπyϑõ3Ïtø:$#uρ |=≈tGÅ3ø9$# ãΝßγßϑÏk=yèãƒuρ öΝÍκ@Ïj.t“ãƒuρ ϵÏG≈tƒ#u öΝÍκö@n=tã (#θè=÷Ftƒ öΝåκ÷]ÏiΒ Zωθß™u‘ z↵Íh‹ÏiΒW{$# ’Îû y]yèt/ “Ï%©!$# uθèδ
∩⊄∪ &Î7•Β 9≅≈n=|Ê ’Å∀s9 ã≅ö6s% ÏΒ (#θçΡ%x. βÎ)uρ
((Yeye Ndiye Aliyepeleka Mtume kwa Al-Ummiyyiyna [watu
wasioelewa kusoma wala kuandika] miongoni mwao anawasomea
Aayah Zake na Anawatakasa, na Anawafunze Kitabu [Qur-aan] na
Hikimah [Sunnah], na japo walikuwa kabla katika upotofu
bayana))9
Fadhila za kusoma, kuhifadhi na kuisikiliza Qur-aan ni nyingi kama
zilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Vitabu na makala nyingi
zimeandikwa kuhusiana na hilo; zifuatazo ni baadhi ya fadhila zake
• Kama biashara isiyofilisika:
ZπuŠÏΡŸξtãuρ #uÅ öΝßγ≈uΖø%y—u‘ $£ϑÏΒ (#θà)xΡr&uρ nο4θn=¢Á9$# (#θãΒ$s%r&uρ «!$# |=≈tGÏ. šχθè=÷Gtƒ tÏ%©!$# ¨βÎ)
∩⊄∪ u‘θç7s? ©9 Zοt≈pgÏB šχθã_ötƒ
((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah [Qur-aan], na
wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale
Tuliyowaruzuku kwa siri na [kwa] dhahiri wanataraji tijara
isiyofilisika)) 10
8Al-‘Imraan
(3: 164)
(62: 2)
10Faatwir (35: 29)
9Al-Jumu’ah
7
www.alhidaaya.com
• Mbora Miongoni Mwa Waumini
Bila shaka yoyote ile yenye ubora au uzuri wa kitu huthibiti kwa
sababu hii au ile au kwa kufungamana na mwenye hicho kitu;
na ubora au uzuri wa Qur-aan ni kwa kuwa ni Maneno ya
Aliyembora kabisa; na kuna ubora gani ulimwengu huu kuliko
mtu kujifunza au
kufundisha Maneno ya Allaah; jambo
alilolianza
mwalimu aliyebora kuliko wote hapa duniani
ambaye ni Mtume ( ). Hivyo hakuna kazi wala
amali iliyobora kuliko ile kazi au amali aliyoifanya Mtume ( ) ambayo ni kusoma na kuisomesha Qur-aan kama
ilivyothibiti katika Hadiyth:
((* + +$ , - . ,
/ )) :
! " #$ % & ' ! Impokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (0 123)
kwamba Mtume ( ) amesema: ((Mbora wenu ni
yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha))11
• Thawabu Kwa Kila Herufi Moja:
Kusoma au kusomesha Qur-aan ni ‘ibaadah kama ilivyotangulia;
na ni ‘ibaadah yenye kumpatia mwenye kuabudu malipo
makubwa kama itafungamana na sharti kubwa katika masharti
ya ‘ibaadah katika Uislamu ambalo ni ikhlaasw. Hivyo mwenye
kuisoma Qur-aan kwa nia safi huwa na matarajio ya malipo
kama haya yaliyothibiti katika Hadiyth ya ibn Mas’uud (0 123)
kwamba Mtume ( ) amesema:
55 5 + 5 5 5
<6 = #> 5#?. 6 5 @ $ 5A B0" 4 9 :;
4 56 - 75 8
4B0"
9 A ,C D#E - . #FC 9 6 ,< - . ))
5 4 9 = 8
((8
4 9 4 . 8
4 4 9
((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata
hasanah [jema] moja, na kila hasanah moja ni sawa na
11Al-Bukhaariy,
Muslim, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, Ahmad
8
www.alhidaaya.com
thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja,
bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi
moja))12
• Kuwa Miongoni
Awapendao:
Mwa
Watu
Wake
Allaah
(‫وتعالى‬
‫)سبحانه‬
Qur-aan kama tuaminivo ni Maneno ya Allaah, hivyo mwenye
kushikamana nayo iwe kwa kuisoma na vyenginevyo huwa ni
miongoni mwa watu Wake Allaah Anaowapenda. Imethibiti
hili katika Hadiyth ifuatayo:
5 5 +5 5
$ ( * ! + ,
5 0 - .5 -
((G#+
)
.
H 6 + I)) : - ! 5 JH 6 H )) :
((E
+ #/ 5 + J H 6 0 ! * .
$ 1 .
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (0 123) kwamba
Mtume ( ) amesema ((Allaah Anao watu wa aina
mbili Anaowapenda katika watu)). Wakamuuliza, ee Mtume
wa Allaah, ni nani hao? Akasema: ((Hao ni watu wa Qur-aan
na ni watu wa Allaah Awapendao))13
• Thawabu Hata Kwa Mwenye Kuisoma Kwa Mashaka:
Wengi huachana na kitu au jambo lolole lile khasa likiwa
linahusiana na kusoma au kutafuta elimu ikiwa litakuwa lina
taabu na mashaka ndani yake; isipokuwa kwa wenye moyo
mgumu na subira isiyoelezeka au lengo analotaka kulifikia au
malipo aliyoahidiwa kuyapata; kwa kuelewa hayo basi
Mtume ( 2 3 ) hakutaka Waislamu wakate tamaa au
waache mara moja kusoma au kujifunza kusoma Qur-aan
kwa kisingizio kuwa lugha yenyewe kwanza mtu haielewi, pili
hata akisoma huwa anadodosa dodosa na pengine watu
kumcheka maana anasoma kwa mashaka na taabu kubwa;
kwa kuelewa hayo Mtume ( ) aliwatia nguvu
Waislamu kwa kuwahakikishia kuwa malipo yako kwa kila
12At-Tirimidhiy
13Ahmad,
Ibn Maajah
9
www.alhidaaya.com
msomaji wa Qur-aan hata kama anapata mashaka ikiwa ana
ikhlaasw:
5K3,& 57
5
5 5 + L. $ 5
5 6 7 ! #5A H#* )) : K "
.
4
5 M6 ON #P 5 ;H 5 C5 LE$ ,EE,Q 6 ,Q RS5 +
((
Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (#>0 123) kwamba Mtume
( ) amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma
Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah,
watukufu, wema. Na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa
mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira
mara mbili))14
• Harufu Nzuri Na Ladha Nzuri Kwa Anayeisoma Qur-aan:
Mtume ( ) ametofautisha mfano wa Muumini
anayesoma
na
asiyesoma
Qur-aan
katika
Hadiyth
iliyopokelewa toka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy(0 123) :
5
5 5
RS5 + -5 .5T * J ?. U
35 BM+ ,X J5 ?* 6 ,Q RS+ -5 .T * J ?. ))
4 V
W #> * $ W U
4 V
W #> Q
5
((;4 9 #> * $ W #> YQ
35 = K *+ E J5 ?* 6 ,Q =
Imepokelewa kutoka kwa ((Mfano wa Muumini ambaye
anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah15; harufu yake
nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma
Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini
zina ladha tamu))16
14Al-Bukhaariy
na Muslim
linalofanana na ndimu lenye rangi ya orenji inayokaribia rangi ya
dhahabu, linajulikana kama tufaha la ki-Ajemi. Lina harufu nzuri kabisa.
15Tunda
16Al-Bukhaariy,
Muslim, Ahmad, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, Ibn Maajah
10
www.alhidaaya.com
• Qur-aan Ni Kiombezi Siku Ya Qiyaamah:
Mwenye kupenda kutafuta marafiki na maswahiba wa kweli
na wakumfaa basi afanye usahiba na Qur-aan kwani haina
kawaida ya kumtupa mkono swahiba wake wakati wa shida
na fazaa:
9 :1 +%Z5C [ ,<)) :.
$ 4; .
"< 0
5 * * - 8- !
5 5 5 5
((5 5A# X #$
F P B.# ; ,Q 15\Q
Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliyy (0 123)
ambaye amesema: “Nimemskia Mtume ( )
akisema: ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah
ikimuombea aliyekuwa swahiba wake [mwenye kuisoma]))17
• Qur-aan Humnyanyua Mtu:
5 S >5A LC,Q + + 5I)) :
5 E7
L ]
@ Q #.F ; ,<6 D#
= % > * - ? & ((-Q
5 5A
5 /
'Umar (0 123) amesema: “Mtume wenu amesema: ((Allaah
Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki [Qur-aan] na
Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki))18
• Qur-aan Humpandisha Mtu Daraja Ya Pepo:
5 5 :#
5 U
^5 3 6 ,< ! ?( & ! + @
! ,Q)) :
5 9#_
5 c 0 5 `
((#> 5A 6 , BeQ 5 /
Ea5 0 . + Z5C #
,%cb 15C J V , d
0 #* J V3
Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar (#*>0 123)
kwamba Mtume ( ) amesema: ((Huambiwa
swahiba wa Qur-aan [aliyeshikamana na Qur-aan]: “Soma na
panda [juu katika daraja za Pepo] na uisome kwa 'Tartiyl'
17
18
Muslim
Muslim Ibn Maajah, Ahmad
11
www.alhidaaya.com
[ipasavyo kwa tajwiyd] kama ulivyokuwa ukiisoma ulipokuwa
duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika Aayah
ya mwisho utakayoisoma))19
• Huteremka Malaika Kwa Utulivu Na Rahmah Kwa Wanaosoma
Qur-aan:
$ 5 ,A -.5 d
e ,A 15C 4;,< L*EM
f;
A?:1?0 8- ! #. )) : .
5
5
> ,E + 9 B* 9 + > ,E
@5 g B0
75 "
+ >5 d
a ,% =+5I > ,0,
,A %; 3 c E,Q 5 + D#
E ;,E ,Q +
5
5
((hc 0 5 - *
C + H i B7 j! * Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (0 123) kwamba
Mtume ( ) amesema ((Hawakusanyiki pamoja
watu katika miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma
kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila
huwateremkia utulivu na hufunikwa na Rahmah na Malaika
huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya [Malaika]
aliokuwa nao))20
L -?9 :I ,M?N
J L -?9 :I , ?:I 4
J K > ,B@+? * C -?9 :1 5D : . 0 & ::+ E( F
G ! + @ -4
- !
R I " -$ S . :I 5 <T U '* K VI R :> 4
.F
D 1- 4
J
& 9 :I W X YZ % - 4
6[ I" :@P - C 4
."0 $ - * \ G .]
'* J ? ^? _< @ a:I" :
. $ `
$ 1 :4 9 :I
9 :I .""?:I 4
J K > b@+? * C -?:- U c. J ! * 5 G $ - & ::+ .
$
9 :I ."F
((e ]
9 - A 6 ,<)) : D 1- 4
J L `
-?9 :I" :
.
$
< ((e ]
9 :I ."F
9 - A 6 ,<)) : D 1- 4
J L `
-?9 :I" ::#
.
R :* D
1? W X % d 4
((e ]
$
9 - A 6 ,<)) : I?e
I" :
.
.
C 4
$ 9 :I ."0 $ - * \ G .]
'* - R I 5 <T U '* 4
J ? ^? _< 1-?:I ,BYZ % - 4
6N
19At-Tirmidhiy,
20
Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad
Muslim Abu Daawuwd, Ibn Maajah , Ahmad
12
www.alhidaaya.com
G#+
&
%# B7 5j! * `
6 ,< ; `
L *5 E" d
5)) : X f
0 #H ,Q d
(( > ,0 .5 5EE" #.
Imepokelewa kutoka kwa Usayd bin Khudhwayr, kwamba
alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad21 yake akashtuka
farasi wake. Akasoma, kisha
akashtuka
tena, akasoma
kisha akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije
kumkanyaga Yahya (mwanawe). Nikainuka kumwendea
(farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama
kina
kandili
kikipanda
mbinguni
hadi
kikapotea.
Nikamwendea Mtume ( ) siku ya pili
nikwamwambia:
“Ee Mjumbe wa Allaah. Jana usiku
nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi
wangu alishtuka! Mtume ( ) akasema: ((Soma Ibn
Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Mtume
( ) akasema: ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema:
Nilisoma lakini alishtuka tena. Mtume ( ) akasema
((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema niliondoka kwani Yahya
alikuwa karibu naye, nikahofu asimkanyage. Nikaona kama
kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Akasema
Mtume ( ): ((Hao ni Malaika walikuwa
wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi watu
wangelikiona kisingelipotea))22
• Kuhifadhi Na Kujifunza Maana Ya Qur-aan Ni Bora Kuliko
Mapambo Ya Dunia:
$ ^?N U
9 :I 5 fe
< C ! g b 5 Q 7 bQ6)) :
.
?( * ! + 5 9 ! e
5 5 $ 5I 6 #
L5 k< = e m5I 5 g 15C -5 Q# .; -5 ,E,<#05A 0 .5 1 5\
,C ^
kA 5I ; ,Q J+ c l,Q 6
< g .
6 ,Q 6 $ ,
,C c5 n5 " * 5I c 9
)
$ 1 9 :I ((e 953
K h
6 c l,Q ! C6)) :
5
5 5 E5 -.5 -5 ,E,Q
e !m -.5 ,
/ o
- .5 4 ,
/ L4 A3 6 o
4 4 !m -5 ,E,<#% - . 4 ,
/ J+ M a+ + D#
5 - .5 -+ H5 q5 c 6 - .5 Le A3 6
((J5 5Ap
21
22
Sehemu ya mifugo ya farasi
Al-Bukhaariy, Muslim
13
www.alhidaaya.com
Imepokelewa toka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (0 123) ambaye
amesema: “Mtume ( ) alitujia wakati tulikuwa
katika Swuffah23 akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu
anayetaka kwenda soko la Butw-haan24 au [soko] la Al'Aqiyq25 na akapata humo ngamia wawili wakubwa na
waliyonona bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?))
Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo.
Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu msikitini akajifunze
au asome Aayah mbili katika kitabu cha Allaah ‫ عزوجل‬basi
akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia wawili. Na Aayah tatu ni
bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko
ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa
ngamia))26
• Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Huvalishwa Taji Siku Ya Qiyaamah:
D
,
,C B5 .# 5 ; ,Q [1n5 Q)) :
V 3 #Q :;
! A?:1?0 8- ! 5V
5 V 3 #Q ::;
u
,Q + m B5 . 7 B+9 s
,Q + m B5 . 7 r#
V 3 #Q ::;
3 D
s
&,
,C ,hq t D
&,
,C ,9
e
5 a , .O 3 6,< : :#
((FB0"
,
,C 0 2
,
,C 0 9 BQ JV 7 A q
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (0 123) kwamba,
Mtume ( ) amesema: ((Qur-aan itakuja siku ya
Qiyaamah na itasema: “Ee Mola, Mpambe” [Mwenye
kuhifadhi Qur-aan]. Kisha atavalishwa taji. Kisha [Qur-aan]
itasema: “Ee Mola, muongeze”. Kisha huyo mtu atavishwa
nguo ya heshim. Kisha itasema: “Ee Mola Ridhika naye”.
Allaah, Ataridhika naye. Kisha ataambiwa: “Soma na panda”.
23
Sehemu katika Msikiti wa Mtume ( 2 3 ) waliyokuwa wakikaa
Maswahaba ambao hali zao walikuwa ni masikini.
24 Bonde lilioko Kusini mwa mji wa Madiyna kuelekea upande wa Magharibi
karibu na Jabali la Sal’. Mtume ( 2 3 ) alitawadha katika bonde hili siku
ya vita vya Khandaq
25 Bonde maarufu kabisa katika mjia wa Madiyna au eneo la Al-Hijaaz yote. Liko
umbali wa maili kilometa mia Kusini na linaelekea upande wa Mashariki.
Linajulikana kuwa ni ‘Bonde lenye Baraka’.
26Muslim,
Abu Daawuwd, Ahmad
14
www.alhidaaya.com
Atapokea thawabu
[atakayosoma]))27
zaidi
ya
mema
kwa
kila
Aayah
• Mwenye Qur-aan Zaidi Huwa Na Mwanga Kaburini:
J? j:+ k&l % d .
@( G
$ % - @ ! + ?+J !
- :i: ! * j
- > Ep - KVI ((
m
5 5 SF / 6 ,? 6 #*>,bQ6)) :.
( @ C *
9 :1 L @( G
@ o@G
. :n C
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (0 123) kwamba alikuwa
Mtume ( ) akiwakusanya watu wawili waliokufa
katika vita vya Uhud katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani
katika hao mwenye ujuzi
zaidi
wa
Qur-aan?))
Anapojulishwa mmoja
kati
ya
hao,
humtanguliza
28
mwanandani))
27At-Tirmidhy
na Al-Haakim
An Nasaaiy
28Al-Bukhaariy,
15
www.alhidaaya.com
04-Umri Bora Wa Kuhifadhi Qur-aan
Umri mzuri utakaofanya sahali kuihifadhi Qur-aan ni baina ya miaka
mitano hadi ishirini na tatu; bali ni bora zaidi kuihifadhi utotoni kabla
ya kufikia umri wa kubaleghe, kwani wakati huo vijana
hushughulishwa na dunia, hasa zama hizi zilizojaa fitnah huwa si
wepesi kuepukana nazo ila tu kwa Rahma ya Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬.
Anapokuwa angali mtoto, kuhifadhi chochote kichwani huwa ni
sahali kwa sababu bongo huwa na kumbukumbu nzuri bado na si
wepesi kusahau anachokihifadhi. Imesemekana kwamba:
5 ,+0# 5 &75 15C 5 ,+0# 5 l_
"[5 #* v
5 w5 n v
5 "
V 15C "Kuhifadhi29 udogoni ni kama nakshi katika jiwe, na kuhifadhi
ukubwani ni kama nakshi katika maji.
Ina maana: Kuchonga au kuchora nakshi katika udongo uliomaji,
mchoro huo hubakia milele kuwa ni alama katika jiwe
litakapokauka. Ama mwenye kuchora katika maji, mchoro huo
hutoweka.
Hata hivyo, haimaanishi kwamba aliyefikia umri mkubwa
haitowezekana kwake kuihifadhi Qur-aan, bali mtu anapopendelea
kutekeleza ‘amali hii tukufu, ajitahidi na Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬
Atamfanyia sahali kwa sababu ahadi ya Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬katika
Suwratul-Qamar haikutofautisha kati ya mtoto au mtu mzima. Wako
walioihifadhi Qur-aan wakiwa na umri zaidi ya miaka arubaini. Bali
imesemekana kwamba mtu aliyefikia miaka zaidi ya sabiini aliweza
kuihifadhi Qur-aan. Muislamu anapaswa awe na iymaan na yakini
kuhusu maneno ya Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬na kuwa na dhana njema,
matumaini na matarajio mazuri daima. Kufanya hivyo, itakupa
nguvu ya azimio la kuihifadhi Qur-aan.
Hivyo ni fursa tukufu kwa Muislamu kuhifadhi Qur-aan. Lakini ikiwa
fursa hii imekupita na sasa inaelekea kwamba huna uwezo wa
kuhifadhi Qur-aan, basi fanya hima na juhudi kuwahifadhisha
watoto wako wakiume na wakike. Usiache fursa hii ikawapita wao
pia kwani furaha yao ya kuhifadhi Qur-aan itakuwa ni furaha na
29
Kauli nyingine imetaja ‘Elimu udogoni ….’
16
www.alhidaaya.com
fakhari kwako na kupata Radhi za Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬na utakuwa
umeshajitangulizia Aakhera akiba.
05- Nasaha Za Kuhifadhi Qur-aan
Kabla ya kuanza kuhifadhi Qur-aan jitayarishe kutekeleza nasaha
zifautazo:
• Kutia Niyya Safi (Ikhlaasw)
Anza na kutia niyyah ya dhati kwamba unakusudia kuhifadhi
Qur-aan kwa ajili ya kupata Radhi za Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬na
kutegemea fadhila na malipo yake, na hivi ndivyo inavyopasa
katika ‘ibaada na amali zote.
• Azimio la nguvu bila ya kukata tamaa.
Weka azimio la nguvu, usichoke, usikate tamaa wala
usivunjike moyo hasa pale utakapoona kwamba unazorota
katika baadhi ya Aayah au Suwrah utakazoziona ngumu.
Chukua mfano wa anayetaka kupanda mlima, akaupanda
pole pole hadi kufikia kileleni. Hivyo basi japokuwa utakuwa
unahifadhi kidogo kidogo, endelea usiache na kumbuka kauli
ya Mtume (‫)صلى ﷲ عليه وآله وسلم‬:
qfi*
5 5 q#. 5 5I -5 QVc U
((&9#
+ 9
6 # ,;b* +E9 + Jb * Q = ...))
(…Allaah Hachoki [kulipa thawabu] mpaka mchoke
wenyewe. Na ‘Ibaadah Aipendayo zaidi ni ile inayodumishwa
na mtendaji)).30
• Kuomba du'aa
Muombe Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬Akupe tawfiyq ya kuhifadhi
maneno Yake. Usiache kuomba kila mara. Tumia Wasiylah31
na nyakati za kukubaliwa du'aa.
30
31
Al-Bukhaariy na Muslim.
Kuikurubisha kwa Allaah ( ) kwa ‘ibaadah
17
www.alhidaaya.com
• Tambua Fadhila za kusoma na kuhifadhi Qur-aan
Soma fadhila hizo upate hima ya kuzichuma na ikupe azimio
la nguvu.
• Kubakia katika Taqwa
Anasema Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬:
〈 3 ª!$# ãΝà6ßϑÏk=yèãƒuρ ( ©!$# (#θà)¨?$#uρ 
((Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzen))32
Kwa hiyo jisafishe kwanza na madhambi kwa kuomba
maghfirah na kutubia kwa Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬, kisha jiepushe na
maasi yote kwani maasi yanamzuia mja kushika maneno ya
Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬. Ibn Mas-‘uwd (‫ )رضي ﷲ عنه‬amesema:
5
5 QU
&
_
e %S 5A $ J M + +5I
"Hakika
mtu
anazozitenda"
hunyimwa
elimu
kwa
dhambi
Imaam Ash-Shaafi'iy (‫ )رحمه ﷲ‬alikuwa mwepesi wa kuhifadhi
Qur-aan lakini Qur-aan ilipokuwa nzito kuihifadhi alisema:
5 5 Le 5 I f
5
5
5
5
5
; 7 P
z , I 1%c P 3\ C ,1y 9 [;
$ + \A 1% ,&/ 6 . 1#$*
5 $5 {c > ,Q = 5 3;% ,3;%
1#
4
"Nililalamika kwa Wakiy’i kuhusu kushindwa kuhifadhi Qur-aan
akaninasihi kuacha maasi na akanijulisha kuwa nuru ya elimu
na nuru ya Allaah haimfikii mwenye kuasi"
• Kutoshughulika na anasa za dunia
32
Al-Baqarah (2: 282)
18
www.alhidaaya.com
Inampasa mwenye kutaka kuhifadhi Qur-aan atumie muda
wake wote kwa ajili ya kuhifahdi Qur-aan. Ajitenge na anasa za
dunia asizichanganye na kazi hii, ili akili na moyo wake upate
utulivu kwa ajili ya hifdhwul-Qur-aan. Watu hupoteza wakati wao
mwingi kushughulika na mambo ya upuuzi yasiyomzidishia
Iymaan wala kumfaa Akhera yake. Fitnah zimekuwa nyingi na
nyenzo zake zimekithiri; mitandao, televisheni, simu za mkono na
huduma zake n.k. Wengineo hukaa mabarazani kwa maongezi
au michezo ya karata n.k. Anayechanganya anasa, upuuzi n.k.
na huku akitaka kuhifadhi Qur-aan hatoweza kabisa kwani
Anasema Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬:
〈 4 µÏ ùÏ θö _
y ’ûÎ 
É
÷ 7t =ù %s ΒiÏ ≅
9 _
ã t 9Ï !
ª #$ ≅
Ÿ èy _
y $Β¨ 
Allaah Hakujaalia mtu yeyote nyoyo mbili kifuani mwake33
• Kuipa Hifdhwul-Qur-aan Kiupambele
Katika ratiba za siku maishani mwako, lazima uipe hifdhwulQur-aan kiupambele. Jiwekee wakati maalumu kila siku uwe
kwa ajili ya kuhifadhi Qur-aan tu. Wakati bora kabisa
uliotambulika kuwa ni muwafaka kuihifadhi Qur-aan ni nyakati
za usiku ambako kuna ukimya na utulivu. Bali wakati mzuri
kabisa ni kabla ya Alfajiri au baada ya kuswali tu Alfajiri kwa
sababu hapo bongo bado liko freshi na liko tayari kupokea na
kuhifadhi kinachosomwa. Hilo limetambulikana kutokana na
uzeofu wa waliohifadhi Qur-aan na jambo hilo halina shaka
kwani kulingana na mchana, ni tofauti kabisa kwa sababu
mchana kuna harakati nyingi ambazo zinaweza kukukatiza
hifdhw yako; mfano watu ingia toka, simu n.k.
• Jifunze Kwanza Kuisoma Qur-aan Bila Ya Makosa
Inapasa mwenye kutaka kuhifadhi Qur-aan kwanza ajifunze
kuisoma Qur-aan sawa sawa bila ya makosa kwani
unapohifadhi kosa huwa vigumu baadaye kulirekebisha. Juu
33
Al-Ahzaab: (33: 4)
19
www.alhidaaya.com
ya hivyo kuisoma Qur-aan kimakosa hubadilisha na kupotosha
kauli za Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬.34
• Jifunze Kuisoma Qur-aan Kwa Hukmu Za Tajwiyd
Kusoma kwa kufuata hukmu za Tajwiyd husaidia kutambua
maneno yanayofuatia, mfano baada ya maddum-munfaswil
(madd ya kuachana) utajua tu kwamba neno la pili litakuwa
linaanzia na herufi ya hamza. Vile vile unapojifunza Tajwiyd
ndipo utakapoweza kuisoma Qur-aan kwa kuitamka vizuri
ipasavyo na kuvuta panapotakiwa na kufanya ghunnah35
panapotakiwa n.k na ndipo qiraa-a cha mtu kinapokuwa
kizuri.
• Jifunze Lugha Ya Kiarabu
Muislamu anapaswa kujifunza lugha ya Kiarabu aweze
kufahamu maneno ya Mola wake. Lugha ya Kiarabu
itamsadia pia mwenye kuhifadhi Qur-aan kutambua vipi
kutamka neno linaloanzia au linalofuatia kwa vile maneno
hubadilika kutokana na hukmu za serufi ya lugha ya Kiarabu.36
Waislamu wengi hawatilii hima kujifunza lugha hii tukufu.
Baadhi ya watu wako tayari kulipia gharama kubwa ya
kujifunza lugha nyinginezo na hali lugha ya Kiarabu ndio
iliyowajibika kwanza ili kuweza kufahamu maneno ya Allaah
(‫ )سبحانه وتعالى‬na ya Mtume Wake (‫)صلى ﷲ عليه وآله وسلم‬.
• Tumia Aina Moja Ya Mswahafu
Tumia Mswahafu wa aina moja, usichanganye miswahafu
katika kuhifadh kwa sababu mpangilio wa Suwrah
zinavyoanza na kumalizikia zinatofautiana katika baadhi ya
miswahafu, na hivyo hata Ayaah huwa zimetofautiana katika
kupangika kwake kwenye ukurasa. Utakuta katika aina ya
Mswahafu mmoja Aayah fulani imeanzia juu ya ukurasa, lakini
Aayah hiyo hiyo katika aina nyingine ya Mswahafu
Rejea kitabu cha: Alhidaayah Katika Ahkaam Za Tajwiyd- Mlango wa ‘Makosa
Ya Dhahiri Na Yaliyofichika’
35 Sauti inayaotokea puani
34
20
www.alhidaaya.com
imepangika katikati au chini ya ukurasa. Kutumia aina mbili za
mswahafu kutambabaisha mwenye kuhifadhi kwa sababu
mtu anapohifadhi Aayah huwa ni kama taswira (picha)
iliyotua akilini na kubakia katika kumbukumbu. Ndio maana
utamuona aliyehifadhi Qur-aan huwa ni sahali kwake
kutambua Aayah iko sehemu gani ya ukurasa.
• Sikiliza Ulichohifadhi Kila Mara
Mchague Qaariu (msomaji) unayependa kumsikiza urudie
kuzisikiliza Aayah ulokwishazihifadhi hadi zithibitike moyoni. Ni
neema za Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬kwamba imekuwa sahali mno
zama hizi za maendeleo ya teknologia, kupata visaidizi mbali
mbali vya kumsaidia mwanafuzi katika mafunzo ya Dini yake
tena bila ya gharama kubwa.
• Vyakula Na Miti Shamba Ya Kusaidia Kumbukumbu
Imetambulikana kuwa baadhi ya vyakula au miti shamba
husaidia ubongo kuamsha kumbukumbu na kutibu usahaulifu.
Tumia vyakula na miti shamba ifuatayo upate natija nzuri In
Shaa Allaah:
Asali, habbat-sawdaa (haba soda), lozi, tende, majani ya
jarjiyr, zabibu, mafuta ya zaytuni au zaytuni zenyewe, tiyn,
lubaan-adhikr (ubani wa kumbukumbu au ubani wa maji),
nanaa (weka katika chai ukipenda), zaatari, tangawizi,
'arqisus (vijiti fulani vya mitishamba vinaponyesha kifua pia).
Michanganyiko ifuatayo Imetambulikana kuleta manufaa:
• Saga njugu za pistachio, zabibu nyeusi, lozi, lubaan-adhikr
kisha tia katika asali kiasi cha kuchanganyika vitu vyote hivyo
vizuri na kula asubuhi na jioni kijiko kimoja cha chai.
• Loanisha nyuzi chache za zaafarani katika maziwa ya
dafudafu, subiri ilowanike kisha kunywa.
21
www.alhidaaya.com
06- Utaratibu Wa Kuhifadhia Qur-aan
Kuhifadhi Qur-aan inategemea uwezo wa mtu; kuna
wanaoweza kuhifadhi ukurasa mmoja kwa dakika chache tu.
Wengineo huwachukua masaa. Kulingana na uwezo wako,
fuatilia utataribu ufuatao unaotumika zaidi kwa kuwa
umeonekana ni muwafaka na unaoleta najita nzuri.
• Soma Aayah unazotaka kuhifadhi uhakikishe unazisoma sawa
sawa bila ya makosa yoyote.
• Anza kuhifadhi Aayah moja, ikithibitika moyoni, isome mara
kumi.
• Ongeza Aayah ya pili ikithibitika soma mara kumi, kisha rudia
Aayah ya mwanzo na hii ya pili usome mara kumi zote mbili.
• Ongeza Aayah ya tatu uhifadhi, ikithibitika, isome mara kumi,
kisha rudi kuanzia Aayah ya mwanzo, ya pili na hii ya tatu
usome mara kumi zote. Endelea hivyo hivyo kwa kadiri ya
uwezo wako wa kuhifadhi kwa siku kama ni Aayah tatu
utakomea hapo, kama una uwezo wa kuhifadhi zaidi
utaendelea kwa utaratibu huo huo.
• Usiendelee mbele hadi uwe umezithibitisha Aayah
ulizozihifadhi vizuri. Ukifanya kosa urudie kuihifadhi Aayah
yenye kosa hadi kusikuweko na makosa kabisa. Hatimaye
Utakapoweza kuhifadhi ukurasa mzima, usikilizwe na pindi
ukikosea makosa zaidi ya matatu basi urudie kuzihifadhi tena
ukurasa huo mpaka uthibitike. Utaratibu huu wa kurudia tokea
Aayah za mwanzo na kuzirudia kusoma mara kumi husaidia
kukumbuka mfuatano wa Aayah bila ya kuipita moja katikati.
22
www.alhidaaya.com
• Ikiwa unajihifadhisha mwenyewe, ni muhimu upate mtu
akusikilize kila unapothibitisha moyoni Aayah kadhaa
akusikilize pia unapofanya marejeo ya hifdhw ya Suwrah
ulizozihifadhi.
• Soma kwa sauti ya kusikilizika na sio kimya kimya. Ukiwa ni
peke yako, jifungie chumbani uwe huru kuisoma kwa sauti ya
juu.
• Siku ya pili, endelea kuchukua Aayah mpya kadiri uwezavyo.
Zihifadhi kwa utaratibu huo huo.
• Utakapomaliza, fanya marejeo ya kuzisoma Aayah ulizohifadhi
mwanzo yaani jana yake, kisha unganisha na hizi mpya hadi
zote zithibitike moyoni.
• Siku ya tatu endelea hivyo hivyo, kila unapozidi kuhifadhi
ndipo unapozidi kupanua ubongo wako kuweza kuhazini
Aayah nyingi akilini lakini pia ndipo kila unapohitaji muda wa
kurudia Aayah za mwanzo ulizozihifadhi.
• Kuziandika Aayah katika kitabu au ubao ni njia mojawapo
iliyojaribiwa na kuonenakana imeleta natija ya kusaidia hifdhw
ya Qur-aan.
23
www.alhidaaya.com
07-Zingatia Aayah Zinazofanana
Anasema Allaah (‫)سبحانه وتعالى‬:
〈’
u ΤÎ $Ws Β¨ $γ
Y 6Î ≈±
t Ft Β• $6Y ≈Gt .Ï ]
Ï ƒ‰
Ï tp :ø #$ 
z ¡
| m
ô &r Α
t “¨ Ρt !
ª #$ 
Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa; Kitabu (Qur-aan)
zinazoshabihiana (kauli zake kwa uzuri na haki bila kupingana na)
zenye kukaririwa kila mara (bila ya kuchosha)37
Anayehifadhi Qur-aan aghalau hutatizwa na kubabaika katika
Aayah zinazofanana katika Qur-aan. Kufanana kwake huwa ima
kwa kutangulia neno au maneno, au kutofautiana katika herufi au
irabu n.k. Utakapozitambua na kuzihifadhi sawa sawa kauli hizo, basi
utajiepusha na kutatizwa huko In-Shaa-Allaah. Kuna vitabu kwa
lugha ya Kiarabu ambavyo vimetaja Aayah hizo laiti kama
vingefasiriwa vitabu hivyo kwa lugha ya Kiswahili. Mifano michache
ya kauli za Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬zinazofanana ni kama ifautavyo:
• Mfano wa kwanza:
( «!$# Îö&tóÏ9 ϵÎ/ ¨≅Ïδé& !$tΒuρ ...
… Wa maa uhilla bihi lighayri-LLaah38
Aayah hii katika Suwratul Baqarah ni pekee iliyotanguliza neno
la ‘bihi’ kabla ya ‘lighayri-LLaah’ :
Ama kwengineko kama katika Suwratul-Maaidah (5:3)
Suwratul-An-aam (6: 145) Suwratun-Nahl (16:115) imekuwa
tofauti na hiyo Aayah ya Suwratul-Baqarah kwa kuwa neno la
‘bihi’ limekuja baada ya ‘lighayri-LLaah’ .
( ϵÎ/ «!$# Îö&tóÏ9 ¨≅Ïδé& !$tΒuρ
Wa maa uhilla lighayri-LLaah bihi
37
38
Az-Zumar (39: 23)
Al-Baqarah (2: 173)
24
www.alhidaaya.com
Pia katika Suwratun-Nahl haikuanzia na: $! Βt ρu .
• Mfano wa pili:
Zingatia kauli za Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬zifuatazo jinsi zilivyofanana
na kutofautiana:
$oÿÏ3 y7Ï9≡sŒ
3
Èd,y⇔ø9$# Îö&tóÎ/ z↵ÍhŠÎ;¨Ψ9$# šχθè=çGø)tƒuρ «!$# ÏM≈tƒ$t↔Î/ šχρãàõ3tƒ (#θçΡ%x. óΟßγ¯Ρr'Î/ y7Ï9≡sŒ
∩∉⊇∪ šχρ߉tF÷ètƒ (#θçΡ$Ÿ2¨ρ (#θ|Átã
Dhaalika biannahum kaanuw yakfuruwna bi-aayaati-LLaahi
wa yaqtuluwnan-nabiyyiina bighayril-haqq. Dhaalika bimaa
‘aswaw wa kaanuw ya’taduwn39
$yϑÎ/ y7Ï9≡sŒ 4 9d,ym Îö&tóÎ/ u!$uŠÎ;/ΡF{$# tβθè=çGø)tƒuρ «!$# ÏM≈tƒ$t↔Î/ tβρãàõ3tƒ (#θçΡ%x. öΝßγ¯Ρr'Î/ šÏ9≡sŒ
∩⊇⊇⊄∪ tβρ߉tG÷ètƒ (#θçΡ%x.¨ρ (#θ|Átã
Dhaalika biannahum kaanuw yakfuruwna bi-Aayati-LLaahi wa
yaqtuluwnal-anbiyaa-a bighayri haqq. Dhaalika bimaa
‘aswaw wa kaanuw ya’taduwn40
Kauli zifuatazo zimefanana lakini zimetofautiana katika irabu;
ya kwanza imetajwa kwa fat-haa na pili kwa kasra.
ãΝßγn=÷Fs%uρ (#θä9$s% $tΒ Ü=çGõ3oΨy™ ¢ â!$u‹ÏΖøîr& ßøtΥ
w uρ ×&É)sù ©!$# ¨βÎ) (#þθä9$s% šÏ%©!$# tΑöθs% ª!$# yìÏϑy™ ô‰s)©9
9d,ym Îö&tóÎ/ u!$uŠÎ;/ΡF{$#
…Waqatlahumul-anbiyaa41
39
40
41
Al-Baqrah (2: 61)
Aal-‘Imraan (3: 112)
Aal-‘Imraan (3: 181)
25
www.alhidaaya.com
9d,ym Îö&tóÎ/ u!$uŠÎ;/ΡF{$# ãΝÎγÎ=÷Fs%uρ «!$# ÏM≈tƒ$t↔Î/ ΝÏδÌøä.uρ óΟßγs)≈sV‹ÏiΒ ΝÍκÅÕø)tΡ $yϑÎ6sù
…Wa qatlihimul-anbiyaa42
• Mfano wa tatu:
Aayah zilofanana na kutofautiana kidogo katika kauli ya
Allaah ( ) kuhusu Nabii Zakariyyah (rs_ ) na Maryam
mama wa Nabii ‘Iysaa (rs_ ) katika Suwratul-’Imraan:
ã≅yèøtƒ ª!$# šÏ9≡x‹x. tΑ$s% ( ÖÏ%$tã ’ÎAr&tøΒ$#uρ çy9Å6ø9$# zÍ_tón=t/ ô‰s%uρ ÖΝ≈n=äî ’Í< ãβθä3tƒ 4’¯Τr& Éb>u‘ tΑ$s%
â!$t±o„ $tΒ
… kadhaalika-Allaahu Yaf-'alu …..43
4 â!$t±o„ $tΒ ß,è=÷‚tƒ ª!$# Å7Ï9≡x‹Ÿ2 tΑ$s% ( ×|³o0 Í_ó¡|¡ôϑtƒ óΟs9uρ Ó$s!uρ ’Í< ãβθä3tƒ 4’¯Τr& Éb>u‘ ôMs9$s%
… kaadhaliki-LLaahu Yakhluqu ….
• Mfano wa nne:
9≅sWtΒ Èe≅ä. ÏΒ Èβ#uöà)ø9$# #x‹≈yδ ’Îû Ĩ$¨Ζ=Ï9 $oΨøù§|À ô‰s)s9uρ
… lin-naasi fiy haadhal-Qur-aan…44
Hapa tunaona kwamba neno lin-naasi limetangulia. Ama
katika Aayah ifuatayo limekuja baadaye.
4 9≅sWtΒ Èe≅à2 ÏΒ Ä¨$¨Ζ=Ï9 Èβ#uöà)ø9$# #x‹≈yδ ’Îû $oΨøù§|À ô‰s)s9uρ
42
43
44
An-Nisaa (4: 155)
Aal-‘Imraan (3: 40)
Al-Israa (17: 89)
26
www.alhidaaya.com
… fiy haadhal-Qur-aan lin-naasi
Mifano mingi mno imo katika Qur-aan iliyokuwa katika hali kama
hizo, na vinginevyo. Na pia nyingi hutofautiana pale inapomalizika
Aayah; mfano Aayah mbili zinazofuatiana katika Suwratul-Maaidah:
∩∉⊄∪ tβθè=yϑ÷ètƒ (#θçΡ%x. $tΒ š[ø⁄Î6s9
Labi-isa maa kaanuw ya’maluwn45
∩∉⊂∪ tβθãèoΨóÁtƒ (#θçΡ%x. $tΒ š[ø⁄Î6s9
Labi-isa maa kaanuw yaswna'uwn46
Kisha katika Aayah Namba 79 imetofautiana tena:
∩∠∪ šχθè=yèøtƒ (#θçΡ$Ÿ2 $tΒ š[ø⁄Î6s9
Labi-isa maa kaanuw yaf'aluwn47
Zingatia pia Asmaa na Swifaat za Allaah ( ) zinavyomalizika
ambazo mara nyingi zimetajwa mbili mbili, huwa zinatofautiana
mara kwa mara. Asmaa na Swifaat za Allaah ( ) zimekariri
zaidi katika Suwratun-Nisaa. Pia aina za adhabu zinavvyotajwa
mwishoni mwa Aayah. Almuradi darsa hili ni pana mno inahitaji
mijalada ya vitabu! Inatosheleza kwamba anayehifadhi Qur-aan
atambue swala hii na awe makini mwenyewe katika kutambua
kauli na maneno hayo.
45
46
47
Al-Maaidah (5: 62)
Al-Maaidah (5: 63)
Al-Maaidah (5: 79
27
www.alhidaaya.com
08-Kuithibitisha Qur-aan Baada Ya Kuihifadhi
Kuhifadhi Qur-aan si tatizo kama kuithibitisha, kwa sababu mtu
anaweza kuhifadhi ukurasa mmoja chini ya nusu saa, lakini ikiwa
hakuifanyia juhudi kukariri kuisoma hadi ithibitike vyema moyoni,
basi hapo itakuwa ni khasara kubwa kwa kuwa amepoteza juhudi
kubwa na muda wingi kwa jambo ambalo mwishowe halikuthibiti
lengo lake. Nasaha zifuatazo zitakusaidia kuithibitisha hifdhw yako In
Shaa Allaah:
• Dumisha kusoma Qur-aan
Inakupasa ndugu uliyeihifadhi Qur-aan uendelee kuisoma
Qur-aan kila siku, kila mara bila ya kuiacha. Kila siku uweke
muda maalumu uwe khasa kwa ajili ya kuisoma Qur-aan na
isiwe chini ya nusu juzuu kila siku! Na ukiweza kuisoma zaidi
ndivyo utakavyoweza kuithibitisha zaidi. Ipe ratiba hii
kipambele katika kila siku ya maisha yako. Tahadhari kauli
zifautazo z Mtume ( 2 3 ) mojawapo aliyoiapia:
RS5 +; ,C S H c H#
$ ,)) ! .
* 8- ! 5 - .5 #FEb , cb P 6 ; > 5hc5 5A ce *+ . s ,%
((#> 5 15C J5 5Ap
Imepokelewa toka kwa Abu Muwsaa
( 3 "#$): Amesema
Mtume ( 2 3 ): ((Dumisheni kuisoma Qur-aan. Naapa
kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hiyo
(Qur-aan) ni wepesi kukimbia kuliko ngamia anavyochopoka
katika kamba yake))48
J ?. #* +%5I))
#> W6 5I
48
$ % - &R: "# $ ?& ! + !
: .
5 J5 ?* 5
5
5 U
5 9#
5 9#
#> 7 "
5I B5 + $ * J5 5Ap
U
. 6 #> ,
c H#
((d
&H i
Al-Bukhaariy na Muslim
28
www.alhidaaya.com
Imepokelewa toka kwa ibn ‘Umar (&R 3 "#$) kwamba Mtume ( 2 3) amesema: ((Hakika mfano wa aliyehifadhi Qur-aan ni
kama ngamia aliyefungwa, akimfunga atamzuia, na akimuacha
ataenda zake))49
• Kabla ya kulala rudia Aayah ulizozihifadhi
Imejaribiwa na kuonekana kwamba inasaidia kuthibitisha
hifdhw ya Qur-aan kuzisoma Aayah uilizozihifadhi kabla ya
kulala. Bali ni amali bora kabisa kwamba unasoma Qur-aan
kabla ya kulala kwani huenda ikawa ndio amali yako ya
mwisho pindi umeandikiwa kufariki usingizini ukajaaliwa husnulkhaatimah (mwisho mwema) na hivyo ndivyo itakavyokuwa
hali ya kufufuliwa kwako.
• Zisome Aayah ulizozihifadhi katika Swalaah za Sunnah.
Hii ni njia bora kabisa ya kuthibitisha hifdhw yako. Zitume
kwanza Aayah zilizothibitika vizuri moyoni, kisha pole pole
ongezea nyinginezo. Inaruhusiwa kutumia Mswahafu katika
Swalaah za Sunnah, kwa hiyo weka Mswahafu katika rafu
ndefu inayofikia urefu wa mabega yako uweze kuisoma Quraan bila ya kuishika, na pale unapotatizwa na Aayah, upige
jicho kuhakikisha na kujirekebisha.
• Sikiliza Suwrah ulizozihifadhi.
Pia ni njia nyingineyo muwafaka kabisa ya kuithibitisha hifdhw
ya Qur-aan. Isikilize kila wakati kila mahali, kila unapopata
fursa. Sikiliza hata unapokuwa unafanya kazi zako nyinginezo
ingawa inalotakiwa ni kuisikiliza kwa umakini. Imesemekana
kwamba baadhi ya watu wameweza kuihifadhi Qur-aan kwa
kuisikiliza tu. Kuisikiliza Qur-aan itakusaidia pia kujirekebisha
makosa yako na pia utakapomchagua Qaariu mwenye sauti
nzuri inayekupendezea, utaweza nawe kuisoma kwa sauti hiyo
hiyo. .
• Ifundishe Qur-aan
49
Al-Bukhaariy na Muslim
29
www.alhidaaya.com
Kazi hii humsaidia sana mtu kuithibitsha hifdhw yake. Je, kuna
kazi bora zaidi ya kujifunza na kufundisha Qur-aan? Amesema
Mtume ( 2 3 ) katika Hadiyth ya 'Uthmaan bin 'Affaan
( 3 "#$):
((* +
+$ - . / ))
((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha
akaifundisha))50
50
Al-Bukhaariy
30
www.alhidaaya.com
09-Hitimisho:
Tunamuomba Allaah (‫ )سبحانه وتعالى‬Atufanyie sahali katika amali hii
tukufu na Atupe tawfiyq ya kuisoma kwa njia inayomridhisha Yeye
Pekee, na Atuwezeshe kuihifadhi katika vifua vyetu na kuifanyia kazi
maamrisho na makatazo yake na Atutakabalie du’aa zetu zote na
khasa zifuatazo:
5 *H D#Hi #05%a96 [! M #%35c 3;% w#05A;,< L,
5A3 y5 $ J5 $M + >+
#0.;
5 *g
5 #5A #0*93 + > + .#0.;
#% Vi + > + .FB* 9 3 {cF H 3;
Q5 5 7 F % #.#F . 5I #0 $ M
5
5
5
5
FBn+ 9 #0 $ M
35 #> ,+0 [#
% J5 + [#
% ! #0,<t3 #0>5 M #. 0 . #0* V #0
"% #. 0 .
5
.-
+ 3 #Q
*#$ D
5 5
5+ 5
15C #0 Q
+ |/ `
H 6 H -Q
+ > + .`E
+ > +
S J5 H6 - . #0$ M
5 7 J5 $ M
5 _
5
5
,F#
5C3 B5 +0n I ,F#$
5 P B5 .# 5 15C ,F3;% }
V F#"%T . 5 & 1C ,#F0Q5 < #
%cb 5
5 ,
~ 5I ,F#A#n95 FE 5 35 #+0 -.5
5A F#.#. 5I F!
5q #> V f
5]
6 #Q z q;M `
5
. F
5? F#*
5" + 5 5A# 5 ce *+ . #0V
5&% + J+ .-
. X
Ee Allaah Ijaaliye Qur-aan tukufu kuwa ni raha na uchanuzi wa
nyoyo zetu, na nuru ya vifua vyetu, na utatuzi wa huzuni zetu, na
sababu ya kuondoka wahka na dhiki zetu. Ee Allaah, turehemu kwa
Qur-aan na ijaalie iwe ni kiongozi, nuru, Hidaaya na Rahma. Ee
Allaah tukumbushe tunayoyasahu humo, na tufunze tuliyokuwa
hatuayajui, na turuzuku kuisoma usiku na mchana na ijaalie iwe hoja
yetu (isiwe hoja dhidi yetu) ee Mola wa walimwengu.
Ee Allaah tujaalie tuwe watu wa Qur-aan ambao ni watu wako
mahsusi (Uwapendao). Ee Allaah ijaalie Qu-raan kuwa rafiki
mwandani duniani, na kaburini iwe ni yenye kutuliwaza, iwe nuru
katika Asw-Swiraatw, na iwe kiombolezi Siku ya Qiyaamah, na
tuambatane nayo Peponi, na iwe sitara na kizuizi cha Moto. Na iwe
dalili katika kila kheri na kiongozi kwa Ukarimu Wako ee Mbora wa
wanaokirimu. Rahmah na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad
na Maswahaba zake kwa amani za wingi.
31
www.alhidaaya.com
Éb>u‘ ¬! ߉ôϑptø:$#uρ ∩⊇∇⊇∪ šÎ=y™ößϑø9$# ’n?tã íΝ≈n=y™uρ ∩⊇∇⊃∪ šχθàÅÁtƒ $¬Ηxå Í﨓Ïèø9$# Éb>u‘ y7În/‘u z≈ysö6ß™
∩⊇∇⊄∪ šÏϑn=≈yèø9$#
32
www.alhidaaya.com

Podobné dokumenty

24. Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu

24. Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu yamekamilika, na kwamba hakuna haja zaidi ya kuudumisha uponyaji. Ni hatari sana kufikiri kwamba “utunzaji wa baadaye” hauhitajiki. Kumbuka, Yesu alionya: “Angalia umekuwa mzima, usitende dhambi te...

Více